Jumla ya matukio 118 ya ukatili na udhalilishaji wa kijinsia yameripotiwa mwezi wa Mei, 2020. Kulikuwa na waathirika 118 ambao waathirika wanawake ni 40 (asilimia 33.9) na watoto ni 78 sawa na asilimia 66.1, miongoni mwao wasichana ni 57 (asilimia 73.1) na Wavulana ni 21 (asilimia 26.9) (kama inavyoonesha Jedwali namba1.1, 1.2 na 1.3).