Jumla ya matukio 97 ya ukatili na udhalilishaji wa kijinsia yameripotiwa mwezi wa Juni, 2021. Kulikuwa na waathirika 97 ambao waathirika Wanawake ni 9 (asilimia 9.3) na watoto ni 88 sawa na asilimia 90.7, miongoni mwao wasichana ni 77 (asilimia 87.5) na wavulana ni 11 (asilimia 12.5).