Takwimu za ajali barabarani hutoa taarifa za idadi ya ajali zilizotokea, aina ya waathirikana hali ya waathirika baada ya ajali. Takwimu za makosa ya barabarani hutoa taarifa kuhusu makosa ya barabarani ambayo yameainishwa katika makundi mbali mbali.
Lengo kuu la kutolewa toleo hili ni kutoa taarifa za ajali na makosa ya barbarian za ndani ya Zanzibar. Taarifa hizi ni muhimu na hutumika na wapangaji, watunga sera, watoa maamuzi na wasimamizi wa sheria.
Ajali za Barabarani Jumla ya ajali 36 zimeripotiwa mwezi Febuari, 2026. Wilaya ya Kati imeripotiwa kuwa na ajali zaidi, ajali saba (7) sawa na asilimia 19.4 ukilinganisha na wilaya nyingine.
Published on March 23, 2026