Ajali za Barabarani Jumla ya ajali 28 zimeripotiwa mwezi Agosti, 2026. Wilaya ya Kaskazini ‘A’ na Kaskazini ‘B’ zimeripotiwa kuwa na ajali zaidi, ajali tano (5) sawa na asilimia 17.9 kwa kila wilaya ukilinganisha na wilaya nyingine.
Idadi ya ajali za barabarani zilizotokea kwa mwezi Agosti, 2026 zimepungua kwa asilimia 3.4 na kufikia ajali 28 kutoka ajali 29 zilizoripotiwa mwezi Julai 2026.
Mwezi wa Agosti 2026, wilaya ya Kaskazini ‘A’ na Kaskazini ‘B’ zimeripotiwa kuwa na ajali zaidi, ajali tano (5) kwa kila wilaya ikilinganishwa na mwezi wa Julai 2026 ambapo wilaya ya Kaskazini ‘B’ na Magharibi ‘B’ ziliripotiwa kuwa na ajali zaidi (ajali 6 kwa kila wilaya).
Published on September 16, 2026