TOLEO LA TAKWIMU ZA UDHALILISHAJI MWEZI, FEBUARI 2026 image

TOLEO LA TAKWIMU ZA UDHALILISHAJI MWEZI, FEBUARI 2026

Ofisi ya Mtakwimu Mkuu wa Serikali imeandaa utaratibu wa kuimarisha takwimu za jinsia nchini ikiwemo kukusanya na kuchambua takwimu za matukio ya ukatili na udhalilishaji wa kijinsia.

Toleo hili hutolewa kila mwezi ambalo hutoa muhtasari wa takwimu za maeneo mawili ya uhalifu ambazo ni ukatili na udhalilishaji wa kijinsia. Takwimu hizi zinatolewa kwa kutofautiana kwa kijiografia, kimakundi na kijinsia. 

Jumla ya matukio 98 ya ukatili na udhalilishaji wa kijinsia yameripotiwa mwezi wa Febuari, 2026 ambapo waathirika walikuwa 99. Waathirika wengi walikuwa watoto (waathirika 81 sawa na asilimia 81.8), wakifuatiwa na wanawake 17 (asilimia 17.2) na mwanaume mmoja (1) sawa na asilimia 1.0 Miongoni mwa waathirika watoto 81, wasichana walikuwa 66 (asilimia 81.5 ) na wavulana walikuwa 15 (asilimia 18.5)

Published on March 31, 2026