TOLEO LA TAKWIMU ZA UDHALILISHAJI MWEZI, JUNI 2026 image

TOLEO LA TAKWIMU ZA UDHALILISHAJI MWEZI, JUNI 2026

Jumla ya matukio 143 ya ukatili na udhalilishaji wa kijinsia yameripotiwa mwezi wa Juni, 2026 ambapo
waathirika walikuwa 143. Waathirika wengi walikuwa watoto (waathirika 122 sawa na asilimia 85.3),
wakifuatiwa na wanawake 17 (asilimia 11.9) na wanaume walikuwa wanne (4) sawa na asilimia 2.8.
Miongoni mwa waathirika watoto 122, wasichana walikuwa 105 (asilimia 86.1) na wavulana walikuwa 17
sawa na asilimia 13.9 ya waathirika watoto wote.









Published on July 24, 2026